MAJALIWA: VITENDO VYA UHALIFU VIMEENDELEA KUDHIBITIWA NCHINI

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema vyombo vya ulinzi na usalama nchini vimeendelea kufanya kazi ya kudhibiti matukio mbalimbali ya vitendo vya kihalifu ukiwemo wizi wa mifugo. Ameyasema hayo leo (Alhamisi, Septemba 9, 2021) wakati akijibu swali la Mbunge wa Mbulu Vijijini, Flatei Massay katika kipindi cha Maswali ya Papo kwa Papo kwa Waziri Mkuu Bungeni